Timu ya Tanzania Prisons siku ya Jana wamekabidhiwa basi dogo la kisasa lenye thamani ya shilingi milioni 75 na uongozi wa Jeshi la Magereza Tanzania.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee amesema kuwa kwa muda mrefu klabu hiyo haikuwa na usafiri hivyo iliwalazimu Uongozi wa klabu kukodi magari ili kuwafikisha wachezaji wake uwanjani jambo lililochangia kuongeza gharama za uendeshaji wa Klabu.
Hivyo katika makabidhiano ya gari hilo itasaidia kupunguza gharama za usafiri walizokuwa wanatumia kukodi magari na badala yake pesa ile itatumika katika matumizi mengine ya kuinua klabu yao.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.