Home Makala Rais Atoa Ndege Kuisapoti Yanga sc

Rais Atoa Ndege Kuisapoti Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ametoa ndege maalumu kwa ajili ya kusafirisha wachezaji na mashabiki watakaokwenda katika mchezo wa pili wa fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika utakaofanyika nchini Algeria.

Yanga sc watacheza na Usm Algers katika michezo miwili ya fainali wakianzia hapa nyumbani Mei 28 kisha watakwenda ugenini nchini Algeria kwa mchezo wa marudiano utakaofanyika juni 3 mwaka huu.

Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya kombe la shirikisho nchini baada ya kuiondosha Marumo Gallants ya Afrika ya Kusini kwa mabao 4-1 huku Usm Algers ikifanikiwa kuitoa Asec Mimosa kwa mabao 2-0.

banner

mbali na kutoa ndege pia Rais Samia ameongeza hela ya zawadu kwa kila goli litakalofungwa kutoka shilingi milioni 10 mpaka milioni 20 katika hatua hii ya sasa ya fainali.

“Tunapokwenda kwenye fainali ni Sh20 milioni timu ikitoka na ushindi, hii itatoka na ushindi sio watoke 2-1, ila zaidi ya hapo Serikali itatoa ndege kwenda Algeria,”Alisema Rais Samia

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited