59
Beki wa kushoto kutoka Rwanda anayeichezea Rayon Sports,Eric Rutanga kwa sasa ni mali ya Yanga Sc baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ili kuitumikia timu hiyo.
Rutanga amesema kuwa tayari ameshamalizana na Yanga baada ya klabu hiyo kulazimika kumtumia mkataba kwa njia ya mtandao ‘Email’ kwa kuwa mipaka ya Rwanda bado haijafunguliwa.
“Namshukuru Mungu kila kitu kimeenda sawa kama ambavyo nilikuwa nikitarajia, tayari tumeshamalizana na Yanga na nimesaini mkataba wa kuitumikia kwa miaka miwili,hivyo nasubiri mipaka ya Rwanda itakapofunguliwa wanitumie tiketi ya ndege.