Home Makala Samata Arudi Ubeligiji

Samata Arudi Ubeligiji

by Dennis Msotwa
0 comments

Mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samata amejiunga na klabu ya Royal Amtwerp inayoshiriki ligi kuu nchini Ubeligiji akitokea Fc Fernabahce ya nchini Uturuki kwa dau la yuro milioni 4 ambazo ni takribani Bilioni 10 za Kitanzania.

Samata alijiunga na Fernabahce msimu uliopita akiuzwa kutoka Aston Villa ambayo ilimsajili kutoka Krc Genk ya nchini Ubeligiji ambako nako hakudumu kwa muda mrefu baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.

Jana Jumanne Samata alisafiri nchini humo kukamilisha taratibu za vipimo vya afya na leo ametangazwa rasmi kama mchezaji wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ubeligiji.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited