Home Makala Simba Day Kufanyika Septemba 10

Simba Day Kufanyika Septemba 10

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba Sc imetangaza kuwa Sherehe za Simba Day kwa mwaka 2025 zitafanyika Septemba 10, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ambapo mbali na mambo mengine pia kutakua na mchezo wa kirafiki wa kimataifa sambamba na utambulisho wa mastaa wapya.

Siku hiyo maalumu kwa Wanasimba ambayo hufanyika kila mwaka ni mahususi kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Simba kuelekea msimu mpya ambapo mashabiki hupata nafasi ya kuwaona mastaa hao kwa mara ya kwanza wakicheza uwanjani.

Sababu kubwa ya tukio hilo kubwa la mwanzoni mwa msimu klabuni hapo kufanyika katikati ya wiki ni kutokana na ufinyu wa ratiba ambapo mastaa wengi tayari wapo katika timu za Taifa ambazo zinashiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) na punde tu baada ya hapo mastaa hao hao watakwenda katika michuano ya kimataifa ya kalenda ya Fifa.

Subscription Form in-article

banner

Pamoja na kalenda ya Fifa pia pazia la ufunguzi wa ligi kuu nchini linaanza Septemba 16 kwa mechiya ngaoya jamii baina ya klabu ya Yanga Sc na Simba sc hivyo imekua ngumu kuwapata mastaa wote mapema kwa ajili ya tukio hilo.

“ Ratiba inabana kidogo lakini tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata tarehe ya tukio pendwa kwa wana Simba ambalo litakuwa tarehe 10 ya mwezi wa 9 katikati ya wiki huku tukienda kushuhudia wachezaji wetu kuelekea Msimu mpya wa mashindano mbalimbali “.Alisema Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc wakati akihojiwa na moja ya kituo cha Radio nchini.

Simba Day Kufanyika Septemba 10-sportsleo.co.tz

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan alipohudhuria tamasha la Simba day 2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.(Picha na Michuzi blog)

 

Tamasha la Simba day limekua maarufu nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 na aliyekua mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali ambapo kwa miaka yote limekua linafana kwa kujaza mashabiki lukuki uwanjani ambao huja kwa wingi wakiwa katika jezi za klabu hiyo.

Kwa miaka ya karibuni tamasha hilo limekua chanzo cha mapato kwa klabu hiyo ambapo mashabiki hununua jezi na tiketi zenye thamani ya mamilioni kuja kuwaona mastaa wapya waliosajiliwa klabuni hapo.

Msimu huu Simba Sc chini ya kocha Fadlu David imefanya usajili wa mastaa kadhaa wakiwemo Allasane Keita,Rushine De Reuck,Anthony Mligo,Neo Maema,Jonathan Sowah,Mohamed Bajaber,Morice Abraham,Charles Semfuko huku pia wakijiandaa kutangaza mchezaji mwingine wa mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa ambapo taarifa zinadai wanapambana kukamilisha usajili wa Wilson Nangu na Yakub Selemani ambnao tayari dili hizo zipo mwishoni tayari kukamilika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited