Home Makala Simba Day Yafunika

Simba Day Yafunika

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanya tamasha la kufungua msimu mpya la Simba day ambalo limefunika matamasha yote ya michezo nchini likiwemo la watani zao Yanga sc la wiki ya mwananchi.

Tamasha la Simba day ambalo huadhimishwa kila mwaka Augusti nane siku ya sikukuu ya wakulima ambapo kwa mwaka huu limefana kutokana na idadi kubwa ya mashabiki iliyojitokeza pamoja na mpangilio wa matukio katika siku hiyo huku yote yakichagizwa na ushindi wa mabao 2-0 iliyopata timu hiyo dhidi ya St.George ya Ethiopia.

Simba sc iliifunga St.George ya Ethiopia kwa mabao hayo mawili yaliyofungwa na Kibu Dennis katika kipindi cha kwanza na Nelson Okwa kipindi cha pili akimalizia pasi ya Cletous Chama.

banner

Takribani kiasi cha Shilingi milioni 313 zimepatikana katika tamasha hilo la Simba day ambazo zimetokana na viingilio vya mashabiki ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited