Klabu ya Simba Sc imetwaa taji lake la tatu leo ndani ya msimu wa 2019/20 ambayo ilianza na ngao ya jamii, kwa ushindi wa mabao 4-2 mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems.
Ilianza mechi zake 10 za Ligi Kuu Bara chini ya Aussem kisha ikamaliza na Sven ambaye alitwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Leo Agosti 2 ,Simba Sc imetwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo Fc ,fainali iliyoshuhudiwa na mashabiki wengi huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza ambaye alikuwa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.