Home Makala Simba sc Gari Limewaka

Simba sc Gari Limewaka

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga 3-1 Klabu ya Al Ahly Tripoli ya Libya katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili Septemba 22.

Simba sc ilianza ikiwa chini kutokana na kuwa na presha ya matokeo ambapo hali hiyo iliwachanganya wachezaji na kujikita wanafungwa bao dakika ya 17 ya mchezo baada ya mabeki kuzembea kuokoa mpira kichwa na kumkuta mfungaji Mabululu.

Kibu Dennis alisawazisha kwa tiktak dakika ya 36 ya mchezo na kuirudisha Simba sc mchezoni ambapo dakika ya 45+1 ya mchezo Lionel Ateba akafunga bao la pili baada ya mchezaji wa Tripol kutoa pasi fyongo.

banner

Kipindi cha pili kilikua cha vuta nikivute lakini Simba sc ikiendelea kusukuma mashambulizi kwa kasi huku mabadiliko ya kuwaingiza Fabrice Ngoma,Kelvin Kijiri,Beki Chamou Karabou sambamba na Edwin Balua yaliwalipa Simba sc ambapo walifanya shambulizi la kushtukiza na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 90 lililofungwa na Balua kwa shuti kali baada ya kuwazidi maarifa walinzi wa Tripoli.

Simba sc sasa wamefuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo wanasubiri droo itakayofanyika Oktoba 7 ili kujua watakutana na nani katika makundi.

Pia klabu hiyo ilikabidhiwa shilingi milioni 15 ikiwa ni zawadi ya goli la mama kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited