Home Makala Simba Sc Hoi kwa Raja Casablanca

Simba Sc Hoi kwa Raja Casablanca

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Raja Casablanca baada ya kukbali kichapo cha mabao 3-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ikiwa na idadi kubwa ya mashabiki uwanjani hapo Simba sc ilizidiwa karibuni kila eneo la uwanja na Raja Casablanca ambao walicheza kimkakati muda wote wa mchezo wakipania kupata alama tatu licha ya kutokua na umiliki mkubwa wa mpira.

Iliwachukua nusu saa pekee kwa Raja Casablanca kupata bao likifungwa na Hamza Khaba kwa shuti kali lililomshinda kipa Aishi Manula huku pia Soufiane Benjdida akiipatia Raja bao la pili lililowamaliza nguvu ya kupambana Simba sc ambao ni mabingwa mara kumi na nane wa ligi kuu nchini.

banner

Dakika ya 82 Raja waliongeza bao la tatu kwa penati na mpaka dakika tisini za mchezo zilimalizika kwa Raja kupata alama tatu na kufikisha alama sita katika michezo miwili kileleni mwa Kundi C huku Simba sc ikiwa mkiani mwa msimamo wa kundi bila alama yeyote.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited