Klabu ya Simba sc leo itasafiri kutoka mji wa Ismailia ilipofikia na kuweka kambi ya maandalizi ya msimu kwenda Cairo kuivaa klabu ya Haras El Hodood kucheza mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini.
Simba sc italazimika kusafiri kwenda Cairo kuwafuata wenyeji hao ambao ndiko yaliko makao yao makuu huku wakiwa ni mabingwa wa ligi daraja la pili nchini Misri na msimu ujao watashiriki ligi kuu nchini humo.
Mchezo huo utakua ni mchezo wa tatu kwa Simba sc ikiwa walitoka sare ya 1-1 na Ismailia ya nchini humo kisha kuifunga 6-0 timu ya AbuHamad ya nchini humo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Klabu hiyo sasa inaelekea kutimiza wiki ya pili ya maandalizi ya msimu mpya nchini humo ambapo ikirejea itakua na kibarua katika mchezo wa Simba Day siku ya August 8 huku pia siku tano mbele wakiwa na kibarua kikubwa dhidi ya Yanga sc mchezo wa ngao ya jamii.