Klabu ya Simba sc imewasiliana na klabu ya Kaizer Chiefs kuwa haitafanya biashara ya kumuuza winga wao Kibu Denis Prosper ambae anahitajika na klabu hiyo chini ya kocha Nasredine Nabi.
Katika taarifa hiyo klabu hiyo imeeleza kuwa hawana nia ya kumuachia mchezaji huyo kujiunga na Kaizer Chiefs kwakuwa bado wana malengo nae kuelekea msimu ujao ambapo wanaamini jasho la mchezaji huyo linahitaji sana msimu ujao katika mapambano yote watakayoshiriki.
Taarifa za kuaminika ni kuwa Simba SC kupitia viongozi wake hawana nia ya kumuachia Kibu Denis katika dirisha lijalo la uhamisho.
Hata hivyo pamoja na kocha Nasredine Nabi kujiridhisha kuhusu mchango mkubwa wa Kibu Dennis baada ya kumuona katika michezo kadhaa aliyokuwapa hapa nchini sasa inampasa kutafuta mchezaji mwingine kutokana na msimamo huo wa mabosi wa Simba Sc.