Home Soka Simba Sc Yaachana na Inonga

Simba Sc Yaachana na Inonga

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simna sc imefikia makubaliano ya kuachana na beki kisiki Henock Inonga Baka baada ya makubaliano ya pande mbili kufikia muafaka ambapo klabu hiyo imevuna kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia tano za kitanzania.

Simba Sc ilikua na mkataba na Inonga wa mwaka mmoja ambapo staa huyo hakuonyesha kuhitaji kuutumikia mkataba huo baada ya kupata ofa kutoka klabu ya As Far Rabat ya nchini Morroco ambayo iliwasilisha ofa klabuni hapo.

 

banner

Licha ya ofa hiyo kuonekana ni ndogo lakini Simba sc haikua na budi kuikubali kutokana na ukweli kwamba staa huyo hakua na nia wala moyo wa kuipigania klabu hiyo hivyo kuhitaji kukubaliana kumuuza kwenda klabu hiyo.

“Asante sana kwa familia nzima. Nimekuja kusema asante kwa yote mliyonifanyia. Nadhani leo nilitaka kusema kwaheri. Asante familia mtaendelea kubaki moyoni mwangu kila wakati”.Hayo yalikua ni maneno ya Inonga wakati akiaga mashabiki wa klabu ya Simba sc kupitia mtandao wa Instagram.

Inonga amedumu Simba Sc kwa takribani misimu mitatu iliyopita akitokea klabu ya Dc Motema Pembe ya nchini Congo Drc ambayo alijiunga nayo akitokea Fc Renaisance ya nchini Congo alipodumu kwa miaka miwili tangu 2016.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited