Klabu ya Simba sc imeingia nchini Misri katika jiji la Ismailia kwa ajili kambi maalumu ya maandalizi ya msimu mpya (Pre-seasons) ikiwa na mastaa wake wapya wote iliowasajili msimu huu.
Kikosi hicho kimesafiri Julai 8 jioni na tayari sasa kimeshawasili nchini humo kwa ajili ya maandalizi hayo huku benchi la ufundi likiongozwa na kocha Fadlu Davis likitarajiwa kusafiri muda wowote kuanzia sasa baada ya kusalia nchini kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa vibali vya kazi.
Pia katika kikosi hicho mastaa Aishi Manula,Pa Omar Jobe,Babacar Sarr na Sadio Kanoute hawakuungana na kikosi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uvunjaji wa mikataba yao ambapo baadhi watatolewa kwa mkopo hasa Aishi ambae ana ofa kutoka Azam Fc.
Kipa Ayoub Lakred na Kibu Dennis wataungana na timu moja kwa moja kutoka nchini nchi walizopo sasa ambapo Kibu Yupo marekani kwa ajili ya mapumziko baada ya kazi kubwa ya msimu uliopita.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msimu huu Simba Sc imefanya maboresho makubwa ya kikosi chake ikisajili zaidi ya mastaa 12 wa kigeni na wazawa lengo likiwa ni kurudisha ile heshima iliyopotea kwa miaka mitatu sasa.