Home Makala Simba sc Yaipa Ruvu Shooting 4G

Simba sc Yaipa Ruvu Shooting 4G

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa kwanza mnono kwa kuizamisha klabu ya Ruvu Shooting kwa magoli 4-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Simba sc iliwakosa Cletous Chama na Benard Morrison Simba sc iliandika bao la kwanza dakika ya 39 kupitia kwa Kibu Dennis huku Rally Bwallya akifunga bao la pili dakika ya 64 na John Boko alifunga la tatu dakika ya 81 na dakika mbili mbele Henock Inonga alifunga bao nne dakika ya 83 na kuhitimisha ushindi huo mnono.

Bao la Haruna Chanongo likiwa pekee kwa upande wa Ruvu Shooting ambayo ilicheza kwa umakini mkubwa ilikuwa ni dk ya 83 huku wakiwa wamechezea nafasi nyingi za wazi.

banner

Sasa Simba inafikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 22 kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya pili huku Ruvu Shooting ikibakiwa na pointi 22 nafasi ya 13.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited