Uongozi wa klabu ya Simba Sc unafanya mawasiliano ya karibu na shirikisho la mpira nchini (TFF) ikiwezekana wachezaji wao walioko katika majukumu ya timu ya Tanzania (Taifa Stars) baada ya mchezo dhidi ya Morocco waelekee moja kwa moja nchini Misri .
Mabosi wa Simba Sc wanataka kupunguza urefu wa safari na kupunguza uchovu kwa wachezaji hao kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Masry utakaofanyika nchini Misri Aprili 2 2025.
Simba wanaona safari itakuwa ndefu sana kwa wachezaji hao kama watarudi nchini Tanzania halafu waanze safari ya kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo huo.
Mastaa wa klabu hiyo walioko nchini Morocco na Taifa Stars ni Ally Salim , Kibu Denis Shomari Kapombe , Abdulrazack Hamza , Kagoma Yusuph na Mohammed Hussein.
Mchezo utafanyika nchini humo April 2 mwaka huu katika uwanja wa New Suez na kisha marudiano kufanyika jijini Dar es Salaam April 9 2025.
Â