Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilifanya kikao Julai 15 kupitia mwenendo wa matukio mbalimbali ya kufanya maamuzi mbalimbali ambapo Klabu ya Simba sc imepigwa faini ya shilingi milioni tatu kutokana na makosa mbalimbali kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga sc juni 25 2025.
Katika taarifa hiyo kwa umma imeonyesha kuwa Simba sc imepigwa faini hiyo katika makosa matatu ambapo kila kosa moja faini yake ni milioni moja ikiwemo Milioni 1 kwa kushindwa kuhudhuria mkutano wa waandishi wa Habari siku moja kabla ya mchezo na shilingi milioni 1 kwa kutohudhuria kikao cha kitaalamu cha mechi na Shilingi milioni moja kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi siku ya mchezo.
Mchezo huo ambao uliaghirishwa mara mbili kutokana na sintofahamu mbalimbali ambapo klabu hizo zilikua na madai mbalimbali yaliyosababisha bodi ya ligi kuahirisha mara mbili huku ukifanikiwa kuchezwa Juni 25 2025 kwa kusimamiwa na waamuzi wa kigeni kutoka nchini Misri.
Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa Simba SC kukubali kipigo cha mabao 2-0 na kuukosa ubingwa wa ligi kuu ya Nbc kwa miaka minne mfululizo huku wakikubali kufungwa na Yanga sc kwa miaka yote hiyo minne kila wanapokutana.