Home Makala Simba sc Yapigwa Faini Caf

Simba sc Yapigwa Faini Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imepigwa faini ya kiasi cha dola 10000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 23 za kitanzania kwa kuonyesha vitendo vya kishirikina katika mchezo wa robo fainali kombe la shirikisho dhidi ya Orlando Pirates uliofanyika nchini Afrika ya kusini ambapo Simba sc waliondoshwa kwa penati.

Kabla ya mchezo huo kuanza wachezaji wa Simba sc walizunguka duara huku wakiwasha moto katikati kitendo ambacho kilitafasiriwa kuwa ni imani za kishirikina na mamlaka husika.

Hata hivyo katika barua ya Caf imeonyesha kwamba klabu ya Simba sc inaweza kuonyesha nia ya kukata rufaa kutokana na adhabu hiyo ndani ya siku tatu huku ikitakiwa kuwasilisha utetezi wake ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya hukumu hiyo.

banner

Mpaka sasa uongozi wa Simba sc bado haujatoa taarifa yeyote kuhusiana na barua hiyo kutoka Caf huku ikizua mjadala kwa wadau wa soka nchini ambao hawakutegemea adhabu hiyo ingetolewa kutokana na kitendo hicho ambacho walikichukulia kama mchezo wa kuwatoa wapinzani mchezoni.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited