Kikosi cha Simba kimerejea Dar Es Salaam leo Mei 26 kutoka Visiwani Zanzibar baada ya kupoteza taji la kombe la Shirikisho barani Afrika baada kufungwa kwa matokeo ya jumla ya 3-1 dhidi ya Rs Berkane ya nchini Morocco.
Simba sc imerejea mapema jijini Dar es Salaam ambapo Mei 28 itakuwa mwenyeji wa Singida Black Stars katika uwanja wa Kmc Complex katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini.
Simba Sc baada ya mchezo huo wa ligi itasafiri hadi Manyara katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa ambapo Mei 31 itacheza na Singida Black Stars katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la shirikisho la Crdb nchini.
Kikosi cha Singida Black Stars kipo tayari Dar Es Salaam na Kilicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Yanga Sc ili kujipima kwa ajili ya michezo hiyo miwili na Singida Black Stars ilishinda 3-2 dhidi ya Yanga SC kwenye mchezo huo wa Kirafiki.