Home Makala Simba sc Yarudishwa Shamba la Bibi

Simba sc Yarudishwa Shamba la Bibi

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba sc itaendelea kutumia uwanja wa uhuru kama uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakaofanyika kesho Septemba 21.

Awali kulikua na taarifa kuwa klabu hiyo imeomba kuhama na kutumia uwanja wa Chamazi Complex kama uwanja wake wa nyumbani lakini suala hilo imeonekana limekua gumu na kuamua kuendelea kutumia uwanja huo.

Meneja wa Habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally amethibitisha kuwa mchezo huo utafanyika katika uwanja huo kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo aliandika.

banner

“Mchezo wetu wa ligi kuu NBC dhidi ya Coastal Union utapigwa kesho katika dimba la Uhuru Jijini Dar Es Salaam Saa 10:00 Jioni Wana Lunyasi Karibuni Uhuruni”lilisomeka chapisho hilo katika mtandao wa instgram.

Simba sc iliamua kuutumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wake wa nyumbani katika michezo ya ligi kuu baada ya uwanja wa Benjamini Mkapa kufanyiwa matengenezo ambapo utafunguliwa mwezi ujao huku kukiwa na malalamiko kuhusu hali ya uwanja huo hasa kwa wale wanaotamaza mpira kupitia runinga kutopata picha bora za mchezo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited