Home Makala Simba Sc Yasajili Usiku

Simba Sc Yasajili Usiku

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba Sc imekamilisha usajili wake wa Dirisha kubwa la usajili msimu huu kwa kishindo baada ya kuwasajili mastaa Seleman Mwalimu kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Wydad Athletic Club ya nchini Morocco,Yakub Selemani na Wilson Nangu kutoka Jkt Tanzania ambao wamesajiliwa moja kwa moja baada ya kununua mikataba yao katika timu hiyo.

Usajili huo wa dakika chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya agosti 15 mwaka huu umelenga kuziba mapengo yote yaliyokua wazi klabuni hapo ambapo walau sasa kila naasi ina wachezaji wawili au watatu watakaokuwa wakiwania namba katika kikosi hicho kuanzia msimu ujao.

Selemani Mwalimu yeye ameletwa kuchukua nafasi ya Lionel Ateba ambaye yeye anauzwa baada ya kupatikana ofa nzuri ambayo hata mchezaji mwenyewe ameonekana kuvutiwa nayo ambapo sasa muda wowote klabu hiyo itatoa tangazo rasmi la kuachana na staa huyo ambapo imeshindikana kupata mshambuliaji wa kuziba nafasi yake wa kusajiliwa moja kwa moja.

banner

Kumleta Mwalimu ambaye licha ya kuwa ni mzawa lakini tayari ana uzoefu wa michuano mikubwa ambapo amecheza kombe la Dunia la ngazi ya vilabu nchini Marekani mwezi wa sita mwaka huu ambapo sasa ameletwa ili kupata nafasi ya kucheza zaidi na zaidi kwa msimu mzima huku akiwa na faida ya kuwa mzawa ambapo imekua rahisi kukidhi matakwa ya kikanuni kwa wachezaji wa kigeni ambao wanatakiwa kuwa 12 tu.

Simba Sc Yasajili Usiku-sportsleo.co.tz

Kipa Yakub Selemani yeye ameletwa kuchukua nafasi ya kipa Aishi Manula ambaye ametemwa na klabu hiyo kisha kujiunga na Azam Fc ambao wamemsajili mapema msimu huu ambapo Simba sc ilibakiwa na makipa Ally Salim,Hussein Abel na Moussa Camara ambaye amejihakikishia nafasi kikosini humo hivyo mabosi wa klabu hiyo wameona ni vyema wakaleta kipa wa kumpa changamoto kikosini humo.

Yakoub ni kipa ambaye amekua na uhakika wa nafasi alipokua Jkt Tanzania na sasa ana kazi ya kupambana kulinda nafasi yake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ambapo amekua kipa namba moja kikosini humo akianza michezo yote katika hatua ya makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).

Simba Sc Yasajili Usiku-sportsleo.co.tz

Usajili wa beki wa kati Wilson Nangu umelenga kuziba nafasi ya Che Malone Fondoh ambaye ameondoka klabuni hapo ambapo licha ya kuletwa kwa mastaa wa kigeni akiwemo beki Rushine De Reuck ambao watashirikiana na mzawa Abdulrazack Hamza huku Nangu akiwa tayari kwa kuwapa changamoto ya kuwania nafasi endapo mmoja kati yao hatakua na ufanisi zaidi au endapo mmoja kati atapata na majeraha basi wa kuziba nafasi hiyo atakuwepo tayari.

Pia licha ya kufanya usajili huo siku ya Agosti 15 usiku pia klabu hiyo ina mpango wa kuwatoa kwa mkopo mastaa Awesu Awesu,David Kameta na Valentino Mashaka ambao wanaweza kwenda kujiunga na klabu ya Jkt Tanzania kwa mkopo wa msimu mzima ikiwa ni sehemu ya usajili wa Nangu na Yakub lakini mpaka sasa mastaa hao wapo kambini nchini Misri na kikosi hicho.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited