Katika kutoa heshima kwa Jonas Mkude,klabu ya Simba sc imeamua kustaafisha jezi namba 20 iliyokua ikivaliwa na mchezaji huyo ili kutoa heshima kwa staa huyo ambaye wamechana nae hivi karibuni.
Simba sc imeamua kufanya hivyo siku chache baada ya kutangaza rasmi kuwa wameachana na staa huyo huku hali hiyo ikipokelewa tofauti na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo waliokua wakihoji sababu hasa ya kumuacha licha ya kuitumikia klabu hiyo kwa moyo wote kwa takribani miaka 13.
Mkude ameondoka Simba sc ambapo kwa mujibu wa meneja habari wa klabu hiyo Ahmed Ally kuwa uamuzi huo umetokana na mambo ya kiufundi zaidi japo hawakupenda kuachana nae.
“Ameondoka mtu tunayempenda kweli, ameondoka mtoto wetu, mtoto wa nyumbani kwetu. Kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mchezaji tumewahi kumpenda kama Jonas Mkude na tutaendelea kumpenda,”
“Sisi tulitamani Mkude amalizie mpira wake Simba kwani hatutaki kucheza nae akiwa timu nyingine, kwa sababu tukimfunga ataumia na yeye akitufunga ataumia hatuko tayari kumuumiza Mkude wetu,” ameeleza Mkude akiongeza;
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Tumetoa taarifa ya kuachana nae punde tutatoa taarifa ya kumuaga na tutamuaga kwa heshima zote sisi ndo tunatambua zaidi heshima ya Mkude kuliko mtu mwingine yeyote na tutamuaga kwa heshima hiyohiyo,”Alisema Ahmed Ally