Klabu ya Simba Sc imetoa tamko la kutocheza tena mchezo wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga sc endapo mchezo huo hautachezwa Juni 15 2025 kama ilivyopangwa baada ya kughairisha machi 8 mwaka huu.
Katika taarifa hiyo kwa umma klabu hiyo imesisitiza ipo tayari kucheza mchezo huo siku ya jumapili na endapo utasogezwa mbele basi nao hawatacheza mchezo huo.
“Klabu ya Simba inauarifu umma, wanachama na wapenzi wake kuwa itaingia uwanjani siku ya Jumapili, tarehe 15 Juni 2025, kushiriki mchezo namba 184 kama ilivyopangwa na Bodi ya ligi Kuu Tanzania.
Mabadiliko yoyote ya kujaribu kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu”,Ilisema taarifa hiyo.
“Kwa msingi huo, Klabu ya Simba haitashiriki mchezo wowote wa namba 184 isipokuwa ule uliopangwa kuchezwa siku ya Jumapili, tarehe 15 Juni 2025 na
Tunawaomba wanachama na wapenzi wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kuijaza Benjamin Mkapa siku hiyo muhimu ili kuiunga mkono timu yetu.”ilimalizia kusema taarifa hiyo.
Dabi ya Kariakoo awali ilikua ichezeke tangu machi 8 2025 lakini bodi ya ligi nchini iliahirisha mchezo huo kwa sababu ilizodai za kiusalama.