Home Makala Simba sc Yatua Bukoba,Kuwavaa Kagera Sugar

Simba sc Yatua Bukoba,Kuwavaa Kagera Sugar

by Dennis Msotwa
0 comments

Kikosi cha mabingwa mara nne wa ligi kuu nchini Simba sc kimetua mkoani Kagera kuwavaa Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu nchini hapo kesho katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba huku ikipokelewa kwa shangwe na mashabiki mkoani humo.

Kikosi hicho kimetua mkoani humo kikiwa kamili na mastaa wake wote wa kikosi cha kwanza huku mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez akiongoza msafara huo kuhakikisha wanavuna alama tatu ili kupunguza pengo la alama dhidi ya Yanga sc wanaongoza ligi kuu nchini wakiwa na alama 35.

Mashabiki mbalimbali walijitokeza uwanja wa ndege kuwapokea mastaa hao huku Ahmed Ally ambaye ni meneja wa habari akishangiliwa na mashabiki sambamba na mastaa Aishi Manula na Cletous Chama hali iliyoamsha shangwe kwa mashabiki hao baada ya kuwalaki mastaa wa kikosi hicho.

banner

Mchezo huo ulitakiwa kufanyika mwezi uliopita lakini changamoto ya kuugua ugonjwa wa mafua kwa baadhi ya wachezaji wa timu zote mbili zilisababisha mchezo huo kusogezwa mbele hadi kesho.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited