Msafara wa wachezaji na Viongozi wa klabu ya Simba Sc umewasili salama nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika utakaofanyika nchini humo Mei 17 2025.
Simba sc itavaana na Rs Berkane majira ya saa nne usiku katika fainali hiyo ya kwanza itakayofanyika katika uwanja wa Manispaa ya mji wa Berkane majira ya saa nne usiku siku hiyo ya Jumamosi.
Simba sc mbali na wachezaji na viongozi wa klabu hiyo pia imeambatana na viongozi wa Serikali na waandishi wa habari ambao kwa pamoja wamesafiri na ndege maalumu iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mapema baada ya kumaliza mchezo huo Simba sc itarudi nchini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa pili ambao utakua na kombe uwanjani utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Mei 25 2025.