Home Makala Simba sc Yawavimbia CSKA Moscow

Simba sc Yawavimbia CSKA Moscow

by Dennis Msotwa
0 comments

Habib Kyombo alifunga mara mbili na kuufanya mchezo baina ya Simba sc dhidi ya Cska Moscow umalizike kwa sare ya 2-2 baada ya awali warusi hao kuongoza kwa mabao 2-0 waliyofunga mwanzoni kabisa mwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa kirafiki baina ya klabu hizo uliofanyika Abu dhabi falme za kiarabu.

Timu zote mbili zilikua zimeweka kambi ya mafunzo ya kujinoa kwa ajili ya michuano mbalimbali zinashiriki huku Simba sc ikijiweka fiti kwa ajili ya ligi kuu ya Nbc sambamba na ligi ya klabu bingwa barani Afrika hatua ya makundi.

Mabao ya Cska Moscow yalifungwa kipindi cha kwanza huku dakika ya 65 kikosi kizima cha Cska Moscow kilibadilika na kuingiza kingine kumalizia dakika hizo ambapo kiwango bora cha Habib Kyombo na Saido Ntibanzokiza kilibadilisha mchezo huo na kuufanya umalizike kwa 2-2.

banner

Simba sc itarejea nchini Jumanne Januari 16 kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City siku ya Jumatano januari 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited