Home Makala Simba Sc,Saido Kimewaka

Simba Sc,Saido Kimewaka

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc tayari imeonyesha nia ya kumuongezea mkataba mpya staa Saido Ntibanzokiza ambapo tayari pande zote mbili zimekutana kwa ajili ya mazungumzo ya awali huku kila upande ukiwasilisha matakwa yake katika mkataba huo mpya.

Simba sc imepanga kumuongezea mkataba mpya mapema staa huyo kabla ya mwezi Disemba ambapo mkataba wake mpya utakua umeelekea ukingoni baada ya hapo awali kusaini mkataba wa muda wa mwaka mmoja na nusu.

Taarifa za ndani zinadai pamoja na mambo ya maslahi pia ugumu zaidi unakuja katika muda wa mkataba ambapo staa huyo anataka mkataba uwe wa miaka miwili huku klabu hiyo ikitaka kumpa mkataba wa mwaka mmoja pekee jambo ambalo staa huyo hajaliafiki.

banner

Ingawa bado mazungumzo yanaendelea Imefahamika kuwa Saido Ntibazonkiza yeye amegomea mkataba huo na anahitaji mkataba wa Miaka miwili na kuendelea ili asalie ndani ya Simba Sc huku akijinasibu kuhusu kiwango chake alichokionyesha klabuni hapo mpaka sasa.

Simba sc haina budi kumuongezea mkataba mpya staa huyo ambaye msimu uliopita alipata tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu huku tayari msimu huu akiwa amechangia kupatikanaji wa ushindi katika michezo mitano ya ligi kuu kutokana na kuonyesha kiwango bora.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited