Home Makala Simba Yafuzu Kibabe

Simba Yafuzu Kibabe

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga klabu ya Us Gendamarie kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Us Gendamarie waliamua kufunguka huku wakicheza mipira mirefu kumtafuta mshambuliaji Adebayor ambaye alikua katika ulinzi mkali wa mabeki wa Simba sc Henock Inonga na Joash Onyango huku mpaka mapumziko matokeo yakiwa bila kwa bila licha ya Simba sc kupata nafasi nyingi zaidi za kufunga ambazo walikosa kutokana na ubinafsi na kutokujiamini kwa baadhi ya wachezaji ambao walionekana wamepania kufunga wakiongozwa na Pape Osmane Sakho.

Kipindi cha pili Simba sc walifungua akaunti ya mabao kupitia kwa Saido Kanoute aliyefunga kwa shuti kali dakika ya 63 na kurudisha hali ya kujiamini huku Chris Mugalu akifunga mara mbili dakika ya 68 na 78 na mwisho kipa wa Us Gendamarie alijifunga akiwa katika harakati za kumiliki mpira.

banner

Kutokana na ushindi huo Simba sc imefuzu kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa ya pili barani Afrika akiungana na Rs Berkane kutoka kundi D.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited