Klabu ya Simba sc imekamilisha usajili wa beki Kennedy Juma Wilson aliyekua akichezea Singida United kwa mkataba wa miaka miwili ambapo ataitumika klabu hiyo mpaka mwaka 2021.
Beki huyo mrefu na mwenye nguvu amesajiliwa kuja kuchukua nafasi ya Salim Mbonde aliyetemwa na klabu hiyo baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu hivyo pande zote mbili kukubaliana kusitisha mkataba ama nafasi ya Juuko Murshid ambaye taarifa zinadai ataachana na klabu hiyo.
Kenedy amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Singida United aliyoichezea kwa kipindi kirefu tangu iingie ligi kuu ya Tanzania bara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Beki huyo katili aliitwa na kocha Emmanuel Amunike lakini alitemwa katika idadi ya wachezaji waliosafiri na timu hiyo kuelekea nchini Misri katika michuano ya Afcon.