Droo ya kombe la shirikisho la Azam imewakutanisha wababe wa soka la Tanzania Simba na Azam katika hatua ya robo fainali huku mshindi kati yao atakutana na mshindi kati ya Yanga sc dhidi Kagera Sugar.
Droo hiyo iliyofanyika leo ikijumuisha timu za za Simba sc,Yanga sc,Azam Fc,Namungo pamoja na Kagera Sugar,Alliance fc,Sahare Stars na Ndanda fc ambapo Namungo watawakaribisha Alliance huku Sahare All Stars wakiwa wenyeji wa ndanda na Yanga watawavaa Kagera Sugar jijini Dar es salaam.
Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa mwezi juni na mshindi kati ya Namungo na Alliance atakutana na mshindi kati ya Sahare na Ndanda.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.