Klabu ya soka ya Singida Fountain Gate Fc imefungiwa kusajili na shirikisho la soka Duniani (Fifa) mpaka itakapomlipa aliyekua mshambuliaji wa timu hiyo Nicholas Gyan baada ya kuvunja nae mkataba bila kufuata taratibu sahihi.
Klabu hiyo iliachana na mchezaji huyo ambaye mara nyingi alikua anatumika kama beki wa kulia bila kukamilisha baadhi ya malipo yake na hivyo mchezaji huyo kuamua kukimbilia kushtaki katika shirikisho la soka duniani.
Fifa ilitoa siku arobaini na tano kwa Singida FG kuhakikisha imekamilisha malipo hayo lakini klabu hiyo imeshindwa kukamilisha malipo hayo kwa wakati na kusababisha kufungiwa huko kusajili wachezaji wa kimataifa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na adhabu hiyo kutoka Fifa nalo shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limeifungia klabu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wa ndani mpaka pale itakapokamilisha malipo ya fedha hizo kwa mchezaji huyo.