Home Makala Skude Aaandaliwa Kuwaua El-Merrekh

Skude Aaandaliwa Kuwaua El-Merrekh

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa Yanga sc Miguel Gamondi anaangalia uwezekano wa kumtumia mshambulia Mahlatse Makudubela Skudu kama silaha muhimu kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi dhidi ya klabu ya El Merrekh ya Sudan endapo staa huyo akiwa fiti.

Iko hivi kocha huyo ameona kwamba staa wake huyo hajatumika sana msimu huu kutokana na kuwa nje sababu ya majeraha huku wapinzani wakiwa hamjamkariri akicheza pamoja na mastaa wenzie wa Yanga sc kutokana na kukosa takribani michezo yote ya mashindano tangu aumie siku ya mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam Fc.

Kutokana na hilo kocha huyo anaona kuwa sambamba na kuwa na mastaa wengine kama Pacome Zouzou,Aziz KI na wengine ila staa huyo ataongeza kitu cha ziada zaidi kikosini humo.

banner

“Skudu Yuko vizuri sana na amefanya mazoezi yote na timu Kwa ufasaha mkubwa. Ni miongoni mwa wachezaji ninaopanga kuwatumia kwenye ligi ya mabingwa, lakini Kwa Sasa tunatarajia kuwa na mechi ya kirafiki wikendi hii ambayo itanipa picha kamili ya kikosi kizima na utayari wa Skudu kucheza”. alisema Gamondi

Licha ya kwamba ni kocha mpya,mastaa wa Yanga sc wameonyesha kuzishika kwa uharaka mbinu za kocha huyo raia wa Argentina kiasi cha kutoa dozi za mabao 5 katika michezo mitatu tofauti mpaka sasa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited