Home Makala Skudu Kuwakosa Asas Fc

Skudu Kuwakosa Asas Fc

by Sports Leo
0 comments

Winga wa klabu ya Yanga sc Mahlatse Makudubela ataukosa mchezo wa kwanza wa michuano ya kimataifa wa klabu yake ya Yanga sc kutokana na kusafiri kuelekea nchini Afrika ya Kusini kushughulikia hati yake ya kusafiria ambayo inakaribia kuisha.

Skudu ameitumikia klabu yake ya Yanga sc katika mchezo mmoja pekee wa siku ya kilele cha wiki ya mwananchi na baada ya hapo alicheza dakika saba pekee katika mchezo dhidi ya Azam Fc na kuumia hivyo kuikosa mchezo wa fainali ya ngao ya jamii dhidi ya Simba sc.

Mchezaji huyo tayari alishaanza mazoezi na wenzake lakini kocha Miguel Gamondi amempa ruhusa amalize tatizo hilo huku akiitafuta utimamu wa mwili ili akirejea uwanjani asiweze kukosa michezo mingine hasa ile ya kimataifa.

banner

Yanga sc kesho itacheza na Asas Fc ya Djibout katika mchezo wa awali wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo mchezo huo utafayika katika uwanja wa Chamaza Complex jijini Dar es salaam.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited