Home Soka Stars Yaangusha Alama 3 Drc

Stars Yaangusha Alama 3 Drc

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imekubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Dr Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025 uliofanyika Novemba 10 2024 nchini humo.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Hemed Morocco aliamua kuwaanzisha Clement Mzize na Mbwana Samata kama washambuliaji wakisaidiwa na Mudathir Yahaya na Feisal Salum huku kiungo wa ulinzi akiwa Adolph Mtasingwa Bitegeko akisaidiwa na mabeki Dickson Job na Ibrahim Hamad Bacca huku walinzi wa pembeni wakiwa ni Lusajo Mwaikenda na Mohammed Hussein na golini akisimama Kipa Ally Salim.

Drc pamoja na kuanza na mastaa mbalimbali wanaocheza ulaya ilijikuta ikipata wakati mgumu kupata bao mpaka dakika 45 za kwanza zilipokamilika matokeo yakiwa 0-0.

banner

Uzembe wa walinzi wa Stars kushindwa kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Drc na hatimaye kumbabatiza Clement Mzize na kujifunga bao ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo huo.

Baada ya matokeo hayo timu hizo sasa zinajipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Oktoba 15.

Drc ipo kileleni mwa msimamo wa kundi H ambapo sasa imefikisha alama tisa ikishinda michezo yote mitatu na Taifa Stars imesalia katika nafasi ya pili ikiwa na alama nne katika michuano hiyo ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited