Home Makala TFF Yazuia Mechi Za Kirafiki

TFF Yazuia Mechi Za Kirafiki

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la Soka nchini (Tff) limezuia mecho zote za kirafiki za ligi kuu na ligi za daraja la kwanza nchini mpaka hapo litakapotoa utaratibu mpya ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona.

Katika taarifa iliyotumwa na shirikisho hilo kwenda kwa vyombo vya habari inaonyesha kwamba timu husika inayotaka mechi za kirafiki inatakiwa kuwasiliana kwanza na Tff ili kupata mwongozo juu ya kujikinga na Virusi hivyo.

Hilo limefuatia baada ya picha mbalimbali kusambaa zikionyesha baadhi ya michezo ya kirafiki ambapo mashabiki walikua wamekusanyika bila kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo huku shirikisho hilo likibainisha kuwa litakutana na timu ya Yanga,Simba,Kmc na Transtcamp pamoja na Azam fc kujadili suala hilo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited