Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaoanza leo Septemba 6 unakutanisha timu 12 kuvaana katika viwanja tofauti ili kusaka pointi tatu muhimu kwani zote zinahitaji kutwaa taji la ligi kuu bara.
Simba Sc ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu bara wapo ugenini Mbeya kumenyana na Ihefu FC katika uwanja wa Sokoine huku watani wao wa jadi, Yanga Sc watavaana na Tanzania Prisons uwanja wa Mkapa.
Namungo Fc itawakaribisha Coastal Union uwanja wa Majaliwa huku Biashara United ikimalizana na Gwambina Fc uwanja wa Karume.
Dodoma Jiji itamenyana na Mwadui Fc Uwanja wa Jamhuri ,Dodoma huku Mtibwa Sugar wakigalagazana na Ruvu Shooting huko Morogoro uwanja wa Gairo.