Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) limetangaza kufuta tuzo za soka zinazotolewa na Shirikisho hilo mwaka huu kutokana na janga la virusi vya Corona ambazo zilitarajiwa kutolewa jijini Milan nchini Italia, Septemba 2020.
Washindani wawili duniani ambao ni Lionel Messi anayekipiga Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus hawatakuwa na cha kubeba mwaka huu Kwenye kipengele cha mchezaji bora wa mwaka.
Gianni Infantino, ambaye ni Rais wa FIFA amekuwa akiweka wazi msimamo wake kuwa wanachukua tahadhari kubwa dhidi ya janga la virusi vya Corona na kuhusu tuzo za Ballon d’Or ambazo zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu 1956 haijulikani hatma yake mpaka sasa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.