Home Makala Usajili Wa Henderson kupigwa Stop

Usajili Wa Henderson kupigwa Stop

by Sports Leo
0 comments

Manchester United wameamua kuzuia usajili wa moja kwa moja wa kipa wao Dean Henderson kwenda kuichezea timu ya uingereza ya Sheffield United kwani mlinda mlango huyo ameonyesha kiwango kizuri msimu huu hata kuzifanya timu za PSG,Juventus na Chelsea kuvutiwa nae.

United wanaonekana kumtaka Henderson kuwa mbadala wa De Gea japo wanasubiri kwanza azidi kuimarikana kujizolea uzoefu .

Kipa huyo wa timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 21,mkataba wake unamalizika  2022 lakini United wanataka kumpa ofa ya mkataba utakaomuongezea thamani katika timu yao.

banner

Katika rekodi ya mashindano walioshiriki msimu huu ,Henderson amecheza mechi 30 na kuruhusu magoli 24 pia hajaruhusu magoli katika mechi 11 huku De Gea katika  mechi 32 alizocheza magoli 33 yaliruhusiwa katika lango lake na hakufungwa katika mechi 11.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited