Uongozi wa Azam Fc umesema kuwa tayari ukarabati wa Uwanja wa Azam Complex umekamilika kwa asilimia zote ukiwa sawa na ule wa TP Mazembe.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa ubora wa uwanja huo kwa sasa ni wa kimataifa tofauti na ule wa mwanzo,hivyo baada ya ligi kuu kurudi baada ya kusimamishwa ana matumaini makubwa wachezaji wake watafurahia kufanya mazoezi kwenye uwanja huo.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona na wakati ukifanyiwa marekebisho Azam FC walikuwa wanatumia Uwanja wa Uhuru na Taifa kwa mechi zao za nyumbani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
““Uwanja wetu ubora wake upo sawa na ule uwanja wa TP Mazembe ya Congo kwa sasa upo hatua ya kimataifa hivyo tunajivunia kukamilisha ukarabati wetu kwa sasa”alisema Zaka Zakazi.