Mchezo wa hatua ya robo fainali baina ya Simba sc dhidi ya Wydad Ac utakaofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Benjamini Mkapa utaamuliwa kwa usaidizi wa teknolijia ya video maarufu kama Var(Video Assistance Refaree).
Alhamisi wataalamu wa teknolojia hiyo kutoka Misri watawasili nchini tayari kwa kufunga mitambo yao na kuijaribu kwa ajili ya mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayozikutanisha timu hizo zenye mashabiki wengi katika mataifa yao.
Hii itakuwa ni kwa mara ya pili katika Historia kwa VAR kutumika Tanzania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na huku teknoljia hiyo mara zote ikiitanisha Simba SC pekee ambao wamekua na historia ya kufuzu mara kwa mara katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Caf.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.