Home Soka Vital O Yapigwa 4G

Vital O Yapigwa 4G

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Vital O kutoka nchini Burundi imekubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Yanga sc katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya Yanga sc uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Yanga sc ilianza kupata bao la kwanza mapema dakika ya 6 likifungwa kiufundi na Prince Dube baada ya beki wa Vital O kukosea kuokoa pasi ya mpenyezo ya Mudathir Yahaya na mpira kumkuta mfungaji.

Yanga sc licha ya kufanya mashambulizi mengi langoni mwa wenyeji walishindwa kupata bao kutokana na wenyeji hao kukaa nyuma wakijilinda zaidi.

banner

Kipindi cha pili kocha Miguel Gamondi alimuingiza Pacome Zouzoua akichukua nafasi ya Maxi Nzengeli na kuufanya mchezo uongezeke kasi kidogo ambapo mashambulizi hayo yalisababisha bao dakika ya 68 likifungwa na Cletous Chama.

Mabadiliko mengine ya Gamondi ya kuwaingiza Kennedy Musonda na Clement Mzize sambamba na Duke Abuya yaliichangamsha Yanga sc na kupata mabao mawili ya Mzize dakika ya 74 na Stephen Aziz Ki dakika ya 90+3 kwa penati baada ya kuchezewa fault eneo la 18.

Yanga sc pamoja na kuwa mchezo ulifanyika nchini lakini kiitifaki walikua ugenini kutokana na Vital O kuomba kuutumia uwanja wa Chamazi Complex baada ya nchi yao kutokua na uwanja wenye hadhi ya kuchezea michuano ya kimataifa ya Caf.

Mchezo ujao ambao Yanga sc watakua wenyeji utafanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa wikiendi ijayo ambapo mshindi wa jumla atavaana na mshindi baina ya Sc Villa ya Uganda dhidi ya CBD ya nchini Ethiopia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited