Klabu ya Soka ya Al Hilal ya nchini Sudan, imetangaza dau la dola za Kimarekani 600,000 sawa na shilingi bilioni 1.4 za Kitanzania, ili kumnasa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele kwa msimu ujao.
Mayele amekuwa tishio katika upachikaji wa mabao kwa misimu miwili mfululizo katika Ligi Kuu ya NBC na katika mashindano ya kimataifa, tangu aliposalijiwa na Yanga kutokea Klabu ya AS Vita alikokuwa akicheza kwa mkopo.
Yanga sc bado inaweka ngumu kumuachia staa huyo hasa baada ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili miezi kadhaa iliyopita.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mayele amekua na mchango mkubwa katika klabu ya Yanga sc ambapo msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 16 ya ligi na msimu huu tayari ana mabao 16 huku zikiwa zimesalia mechi tano za ligi kuu kumalizika.