Klabu ya Manchester United (Red Devil) imewataka nyota wake waliopo nje ya England kurejea haraka ndani ya siku saba ili kuendelea na majukumu yao kama zamani.
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya klabu za Premier League kuanza mazoezi ili kujiandaa kwa ligi hiyo iliyosimama tangu Machi, mwaka huu kutokana na uwepo wa maambukizi ya virusi visababishwavyo na Corona.