Kiungo wa klabu ya Simba Sc Fabrice Ngoma amefikia makubaliano binafsi ya kujiunga na klabu ya Al-Ittihad Tripoli ya Libya.
Tayari staa huyo amepokea ofa nono ya Mshahara na dau la usajili (Sign-on fee) kutoka Al-Ittihad na tayari amesema ndio ambapo sasa imebaki kwa Simba sc kukubali uhamisho huo.
Kilichobaki ni makubaliano kati ya Simba Sc na Al-Ittihad na kuanzia muda wowote sasa klabu hiyo tajiri ya Libya itatuma ofa Msimbazi kuhusu dau la kununua mkataba wa staa huyo raia wa Congo Drc.
Mkataba wa Ngoma na Simba umebakiza miezi mitano hivyo kisheria anaruhusiwa kuongea na timu yeyote japo amekua akiipa nafasi zaidi Simba sc endapo itahitaji kumuongezea mkataba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Dirisha la usajili la Libya litafungwa mwishoni mwa mwezi huu na Al-Ittihad wanamuhitaji NNgoma mapema ili kukamilisha sajili zao na kama Simba watakubaliana na ofa ya Al-Ittihad basi nyota huyo ataondoka haraka sana.
Baada ya kukamilisha usajili wa Mahmoud Kahraba kutoka Al Ahly,sasa Ittihad wamemgeukia Ngoma.