Klabu ya Coastal Union ya Tanga imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa klabu ya KenGold Fc Kiala Lassa ambaye amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu yake hiyo ya awali.
Kiala Lassa raia wa Congo anauwezo wa kucheza namba nyingi uwanjani kama vile 7, 11 na 10 na amekuwa na msimu bora sana kwenye Kikosi cha KenGold Fc licha ya kushuka daraja lakini alikuwa bora sana kwenye Kikosi hicho.
Coastal union yenyewe ina uhakika wa kusalia katika ligi kuu ya Nbc nchini kutokana na kuwa na alama 31 katika nafasi ya 10 baada ya kucheza jumla ya michezo 28 mpaka sasa ambapo wanahitaji kushinda mchezo mmoja pekee ili kuwa salama zaidi kutocheza michezo ya play offs.