Home Makala Wydad Athletic Safarini Marekani

Wydad Athletic Safarini Marekani

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Wydad Athletic wameanza safari ya kuelekea nchini Marekani tayari kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia la Vilabu ambayo itaanza kutimua vumbi Juni 15, 2025.

Msafara wa mastaa hao unatarajiwa kuwasili nchini humo juni 11 tayari kwa mashindano hayo yenye hadhi ya juu kabisa duniani kwa ngazi ya vilabu.

banner

Aliyekua nyota wa Yanga SC Stephane Aziz Ki na Mtanzania Selemani Mwalimu ni miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kitakachoshiriki Kombe la Dunia la Vilabu.

Wydad Athletic Club ni moja ya vilabu vitatu kutoka barani Afrika ambavyo vinashishiriki michuano hiyo pamoja na Mamelodi Sundowns na Al Ahly Fc ya Misri.

Wydad Athletic Club ipo katika kundi G pamoja na klabu ya Manchester City,Al Ain Fc na Juventus Fc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited