Kwa nafasi Yanga waliyoachwa na Simba ni ngumu kuwafikia kwani kunahitaji juhudi na akili nyingi kutokana na mzigo wa pointi wanazodaiwa na idadi ya mechi walizonazo.
Aidha  itokee Simba wapoteze mechi zao zilizobaki na wao washinde mechi zao zilizobaki jambo ambalo ni mtihani mgumu kufanikiwa hivyo ni heri yaishe kwa upande wa ubingwa.
Yanga ipo nafasi ya tatu na pointi 51 huku mtani wake wa jadi Simba Sc ana pointi 71 ,Yanga imebakiwa na mechi 11 na Simba mechi kumi.
Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimama kutokana na kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea baada ya mwezi mmoja.