Klabu ya Yanga sc sasa imeshindikana baada ya kuendelea kushikiria rekodi yao ya kutofungwa katika ligi kuu nchini katika jumla ya michezo 49 baada ya kufanikiwa kuifunga Mbeya City Fc kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Fiston Mayele.
Yanga sc ikicheza katika uwanja wa nyumbani wa Benjamini Mkapa ilionyesha soka safi huku ikimiliki mchezo kwa asilimia 73 kwa dakika 90 za mchezo na kuwaachia Mbeya City asilimia 37 pekee za umiliki huku ikifikisha alama 32 ikiwa na michezo 12 ya ligi kuu nchini.
baada ya ushindi huo sasa tayari klabu hiyo imewasili mkoani Mbeya ambapo inakwenda kuvaana na klabu ya Ihefu Fc ikitafuta alama tatu ili kufikisha rekodi ya kutofungwa jumla ya michezo 50 ya ligi kuu nchini huku ikiwa na faida ya urejeo ya mastaa wake Aziz Ki na Djugui Diarra ambao sasa watakua na utimamu wa mwili wa kutosha baada ya kuwa na safari ndefu kuwasili nchini wakitokea katika timu zao za taifa.
Pamoja na kutofungwa katika michezo 49 mpaka sasa pia klabu hiyo imefanikiwa kuwa na takwimu nzuri ambapo katika michezo 12 ya ligi kuu msimu huu imefunga jumla ya mabao 23 na kufungwa 6 na ikitengeneza pasi za mabao 19 huku pia ikiwa ndio timu pekee nchini kushinda michezo yake yote ya ugenini ambapo imeshinda michezo 6.