Home Makala Yanga sc Kuipa Simba sc Manoti

Yanga sc Kuipa Simba sc Manoti

by Sports Leo
0 comments

Bilonea kijana wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji amepania kuwapa mastaa wa klabu hiyo kiasi kikubwa cha pesa endapo watafanikiwa kuifunga klabu ya Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu nchini utakaofanyika siku ya Jumapili oktoba 23 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu huku akiwa hashiriki kwa uwazi katika shughuli za soka bilionea huyo wiki iliyopita alijitokeza uwanjani wakati klabu hiyo ikifuzu hatua ya makundi ya kkabu bingwa barani Afrika kwa kuifunga Premero de Augosto kwa 1-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya awali kushinda kwa mabao 3-1 ugenini.

Simba sc itavaana na Yanga sc huku ikihitaji alama tatu ili kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ambapo mpaka sasa inaongoza ligi kwa alama 13 sawa na Yanga sc iliyo katika nafasi ya pili huku wakitofautiana wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa na urejeo wa Bilonea huyo kuongeza nguvu kunatajwa kuwapa mzuka wachezaji na benchi la ufundi la klabu hiyo.

banner

“Familia yangu ya Simba. Mwanzoni mwa msimu wa ligi, niliandika hivi: Kwa ujumla miaka 5 iliyopita imekuwa ya mafanikio kwa Simba. Bajeti iliongezeka mara 5, tulishinda makombe mengi ya ndani na tuliweka alama kimataifa kwa kufika robo fainali tatu za michuano ya Afrika. Najivunia kuweza kusema tupo katika orodha ya vilabu bora 12 Afrika. Hii imekuwa mara ya kwanza Simba kuwa na mwendelezo mzuri katika miaka 86 ya historia yetu. Hakuna kurudi nyuma, tunatakiwa kufanya mabadiliko katika maeneo ambayo tuna madhaifu na kwenda mbele. Mapambano yanaendelea!”Aliandika bilionea huyo hivi karibuni kujivunia kufuzu kwa Simba sc hatua ya makundi.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited