Klabu ya Yanga Sc imekubali ombi la Kaizer Chief kucheza mchezo wa Kirafiki wakati wa Pre Season ambapo mchezo huo utapigwa nchini Afrika Kusini mwezi Julai (7) licha ya awali kusitasita kutoa maamuzi kabla ya kujua ratiba ya Pre Season.
Mabosi wa klabu hizo mbili wana urafiki na msimu huu Rais wa Yanga sc Eng.Hersi Said alikwenda nchini humo kuonana na mabosi wa timu hiyo katika kudumisha urafiki wao na hapo ndipo mazungumzo ya mchezo huo yalipoanza rasmi.
Katika maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 klabu ya Yanga itaweka kambi nje ya nchi tofauti na tulivyowazoea kwa misimu iliyopita ambapo wamekuwa wakibaki katika kambi yao ya kila siku ya Avic Town jijini Dar es salaam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mastaa wa klabu hiyo ambao hivi sasa wapo katika mapumziko wanatarajiwa kurejea kambini mwanzoni mwa mwezi Julai maalumu kabisa kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa huku mpaka sasa kukiwa hakuna uhakika kama timu hiyo itashiriki michuano ya kombe la Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Julai 6 visiwani Zanzibar.