Sports Leo

Yanga Sc Mabingwa Crdb Cup

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua ubingwa wa kombe la shirikisho la Crdb nchini baada ya kuifunga timu ya Singida Black Stars kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Visiwani Zanzibar katika uwanja wa New Amaani Complex.


Mchezo huo uliokua na burudani ya kutosha kutokana na kasi ya mchezo ulikua mgumu kutabiri nani ataibuka na ushindi katika dakika 30 za mwanzo kutokana na kila timu kuwa imara hasa eneo la kiungo ambapo kulikua na vita kali baina ya Khalid Aucho,Mudathir Yahya na Duke Abuya dhidi ya Morice Chukwu,Damaro Camara na Athur Bada.

Clement Mzize alikosa nafasi ya wazi akiwa na kipa Amas Abasogie baada ya Pacome Zouzoua kutoa pasi safi kwake,Jonathan Sowah alikua mwiba mkali kwa mabeki wa Yanga sc kutokana na kasi sambamba na nguvu akinyumbulika ipasavyo.

Duke Abuya alifunga bao la kwanza kwa Yanga sc dakika ya 39 kwa shuti akimalizia mpira uliotemwa na kipa Abasogie alipocheza krosi ya Israel Mwenda na mpira kumkuta mfungaji akiwa huru.
Dakika tano za mwishoni mwa kipindi cha kwanza zilikua mwiba kwa Singida Black Stars kufuatia kukoswakoswa kufungwa mabao mawili ya haraka haraka huku kipa Abasogie akionyesha uimara mkubwa.
Kipindi cha pili kocha David Ouma aliamua kufunguka na kushambulia kwa kasi kubwa akitamani kupata bao la kuswazisha lakini uimara wa mabeki wa Yanga sc sambamba na kipa Djigui Diara ulikua kikwazo kikubwa kwao.


Clement Mzize alifunga bao la pili kwa Yanga sc dakika ya 50 akipokea pasi safi ya Maxi Nzegeli baada ya Khalid Aucho kupora mpira na kuanzisha shambulizi hilo kwa uharaka Zaidi na kuhitimisha rasmi mbio za Singida Black stars kulinyemelea taji hilo.
Kuingia kwa bao hilo kuliwafanya Singida kucharuka na kushambulia kwa kasi kupitia pembeni lakini walikutana na ugumu kutokana na uimara wa Yanga sc ambapo mara kadhaa walifanya mashambulizi ya kushtukiza na kuwakosakosa mara kadhaa.

Dakika tisini za mwamuzi Ahmed Arajiga zilimazika kwa Yanga sc kuibuka mabingwa mara nne mfululizo wa kombe hilo ambapo sasa kwa msimu huu pekee wamechukua mataji matano mfululizo.

Exit mobile version